Burudani

MTV Africa Music Awards 2014 kufanyika Durban, Afrika Kusini

Tuzo za MTV Africa Music (Awards) mwaka huu zitafanyika kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008.
Tuzo zitatolewa June 7. Zitafanyika katika jiji la Durban.

Alex Okosi(VP MTV Africa Networks)
Mkurugenzi Mtendaji wa MTV Networks Africa, Alex Okosi

Video zitakazoshindana ni zile zilizotoka March 20 mwaka jana hadi March 19 mwaka huu. Tuzo hizo zilianzishwa mwaka 2008 na Abuja, Nigeria. Zilianzishwa kusherehekea muziki wa kisasa wa Afrika katika Hip Hop, Hip Life, R&B, Afro Pop, Afro House, Kwaito, Boomba, Bongo Flava, Coupé Décalé, Dancehall, Soul na Rock.

Mwaka uliofuata tuzo hizo zilifanyika Nairobi, Kenya. Zilirejea tena nchini Nigeria mwaka 2010 ambapo wasanii wa Marekani, Eve, Rick Ross na T-Pain walitumbuiza.

Majina ya watakaowania tuzo hizo yatatangazwa April 16.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents