Michezo

Muacheni Tiote apumzike- wakala wake

Wakala wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ivori Coast na klabu ya Beijing Enterprises nchini China, Cheick Tiote aliyefariki dunia wiki iliyopita Emanuele Palladino amewataka waandishi wa habari na wadau wa soka kuacha kujadili kifo cha mchezaji huyo.

Mwili wa Tiote unasafirishwa kuelekea Ivory Coast

Palladino ametoa wito na kusisitiza kuwa huu si wakati wa kuendelea kuhoji kifo chake na badala yake ni wakati wa kuungana na familia ya mchezaji huyo katika maombolezo.

Papiss Cissé aKishindwa kujizuia wakati wa kuuaga mwili wa Tiote

Mwili wa Tiote uliagwa siku ya Jumanne na mwili wake ukitarajiwa kurejeshwa nyumbani kwa ajili ya mazishi.
Cheick Tiote aliichezea timu ya taifa ya Ivori Coast michezo 52 na kuiwezesha kunyakua taji la bara Afrika 2015.

Tiote alianguka ghafla wakati akifanya mazoezi na klabu yake ya Beijing Enterprises

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents