Mubarak wa Misri aachia ngazi

mubarak

Rais wa Misri, Hosni Mubarak ameachia ngazi baada ya kuongoza nchi yake kwa miaka zaidi ya ishirini, kufuatia siku kumi na nane za wananchi wa Misri kuandamana kumuondoa kiongozi huyo.

Makamu wa Rasi wa nchi hiyo, Omar Suleiman alitangaza habari za kiongozi huyo kuachia madaraka ijumaa usiku ambapo alisema Rais huyo amekabidhi madaraka kwa Jeshi la Misri.

Wananchi hasa waliokuwa wameweka kambi Tahrir Square mjini Cairo, walikuwa wenye furaha kubwa pale ambapo walitangaziwa kuondoka kwa aliyekuwa kiongozi wao kwani ndicho walikuwa wamekidhamiria kupitia maandamano yao.

Rais wa Marekani, Barck Obama, ametoa tamko na kusema,’Leo ni siku ya wananchi wa Misri, tunawatakia kila la kheri,’

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents