Burudani

Mubenga amshauri Ommy Dimpoz, ‘Watu wanataka video ya cheche na sio matusi’

Ujumbe wa maqneno mazito aliouandika Ommy Dimpoz ambao unadai kumlenga Diamond wamshtua Mubenga.

Mubenga ambaye aliwahi kuwa meneja wa Dimpoz na pia ni mmiliki wa kampuni ya Bengar Entertement, ameonekana kukerwa na na maneno ya Ommy ambayo ameandika kwenye mtandao wa Instagram Jumatano hii.

Kupitia mtandao wa Instagram, Mubenga ameandika “Omary mdogo wangu maandiko yanasema waheshimu wazazi upate heri na Miaka mingi duniani na mzazi sio mpaka akuzae ata mzazi wa mwenzio pia ni mzazi wako why unamuingiza mama naseb kwenye mambo yenu? Uko ni kukosa adabu wew si unajifanyaga innocent kwa watu kumbe una pretend? Wew sindio uliyeimba nani kama mama imekuwaje leo una watusi wa kina mama? Au ndio stress za Mziki? Watu wanataka video ya cheche na sio kutusi wazazi wa watu usituaribie muziki wetu kama game imekushinda please kaa pembeni pia naomba vyama vyenye dhamana ya muziki vichukue atua kali zidi ya matusi ya omary kwa mama wa diamond ili iwe fundisho kwa wengine ya kwangu ni hayo tu! #supportedbybangerzent #Mazoea link kwenye bio yangu #TUWAHESHIMUWAZAZIWETU.”

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents