Uncategorized

Muda mchache kabla ya kupangwa kwa Droo ya CAF, haya ndiyo mambo 10 usiyofahamu kuhusu timu zilizoingia hatua hii

Wakati wadau na wapenzi wa soka barani Afrika wakisubiria kwa hamu kubwa droo ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika inayotarajiwa kufanyika usiku wa leo huko nchini Misri, haya ni mambo 10 usiyofahamu kuhusiana na timu zilizofanikiwa kutinga hatua hiyo.

Kwanza kabisa kwenye hatua hii ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika, timu zilizokuwa kwenye kundi moja hatua iliyopita ya makundi hawawezi kupangwa pamoja.

Pili, timu zote zilizofanikiwa kuongoza kwenye makundi yao mpaka kufika hatua hii ndizo zitakazoanza kwenye mechi zao au tunaweza kusema zitakuwa wenyeji katika mchezo wa kwanza kabla yao kwenda kumalizia mechi zao ugenini.

Tatu, jumla ya timu hizi nane zilizofanikiwa kufika hatua hii ya robo fainali ya CAF Champions League, klabu nne zimewahi kuchukua ubingwa huu amzo ni Al Ahly (8), TP Mazembe (5), Esperance (3), and Wydad Athletic Club (2) and Mamelodi Sundowns (1).

Nne, kwenye hatua hii kuna timu mbili ndiyo mara yao ya kwanza kuvuka hatua ya makundi na kutinga robo fainali ambazo ni Simba SC ya Tanzania na klabu ya CS Constantine kutoka Algeria

Tano, hakuna timu yoyote kutoka Baraza la vyama vya Soka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kuwahi kutwaa kombe hili, Simba SC inaweza kuvunja mwiko baada ya kushindwa kufanya hivyo mwaka 1972 mbele ya klabu ya Hafia kutoka Guinea. Wakati El Hilal wakishindwa mara mbili mwaka 1987 na 1972, wakati miamba ya soka ya Uganda SC Villa wakipoteza mbele Club Africain mwaka 1991hatua ya fainali.

Sita, klabu ya CS Constantine ndiyo timu kongwe pekee kwenye hatua hii ya robo fainali, imeanzishwa mwaka 1898, mpaka sasa ikiwa na jumla ya miaka 121.

Saba, bingwa mtetezi wa kombe hili klabu ya Esperance inatarajiwa kuutete kama ilivyofanya Al Ahly mwaka (2005 na 2006) na hata walivyochukua mwaka (2012 na 2013); TP Mazembe (1967 na 1968) na ilivyofanikiwa kufanya hivyo mwaka (2009 na 2010), na klabu ya Enyimba ilivyoutwaa mwaka (2003 na 2004).   

Nane, nchi ya Morocco na Tunisia zina timu mbili kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika ambapo kwa upande wa Morocco zipo klabu ya RS Berkane na Hassania Agadir wakati timu za CS Sfaxien na Etoile du Sahel zikitokea Tunisia.

Tisa wakongwe klabu Raja Club Athletic wapo nje ya michuano hii wakati timu kama CS Sfaxien na TP Mazembe zikizidi kupata mafanikio.

Kumi, miamba ya soka kutoka nchini Zambian, Nkana FC wao wakiwa wanajivunia kuwa na rekodi nzuri ya kutokufungwa nyumbani kwenye michuano ya CAF tangu mwaka 1983.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents