MichezoUncategorized

Muda ninao wa kuitumikia TFF – Imani Madega (Video)

Mgombea wa nafasi ya urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Imani Omar Madega amezindua rasmi kampeni zake leo jijini Dar es salaam.

Madega ambaye mwaka 1999 aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala ndani ya klabu ya Dar es salaam Young Africa chini ya uongozi wa Abbas Tarimba amesema kuwa amekuwa akipata shinikizo kutoka sehemu mbalimbali huku akijitathimini na kujiona anaweza kugombea nafasi hiyo katika kuhakikisha analiletea mafanikio soka la Tanzania.

Mgombea huyo ambaye pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa Yanga, amesema kuwa muda wakulitumikia soka anao na hivyo hana kitakachomfanya ashindwe kwenda na wakati katika kutimiza majukumu yake.

Madega aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Pwani mwaka 2004, ameongeza kuwa miongoni mwa mipango yake endapo atapata nafasi ya kuwa rais wa TFF atahakikisha Tanzania inapanda katika viwango vya FIFA angalau kuhakikisha inaingia ndani ya nafasi kuanzia 99 hadi 50.

Imani Omar Madega alishawahi pia kuwa Mjumbe wa kamati ya utendaji wa kwanza baada ya mabadiliko Shirikisho hilo kutoka FAT lilivyokuwa likiitwa hapo awali mpaka TFF chini ya uongozi wa Leodegar Chilla Tenga akiwa na jukumu la kuweka utaratibu na mfumo wa uendeshaji wa soka Tanzania katika kufanya marekebisho ya katiba

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents