Soka saa 24!

Muda wowote Madrid kumtangaza Zidane kama kocha wao, tetesi za kurejea zaenea Hispania

Klabu ya Real Madrid inampango wa kumrejesha aliyekuwa kocha wake, Zinedine Zidane hii ni kwa mujibu wa tetesi za vyombo mbalimbali vya habari nchini Hispania.

Zidane aliachana na klabu hiyo wakati wa majira ya joto baada ya kutokufurahishwa na mipango ya msimu huu.

Rais wa Real Madrid, Florentino Perez anatarajiwa kukutana na mkurugenzi mwenzake majira ya saa 11 alasiri kufanyamazungumzo ya kumpata kocha wa tatu ndani ya msimu huu.

Kwa upande wake Mfaransa, Zidane huyo amenukuliwa akisema kuwa aliamua kuachana na timu hiyo ili kuifanya inaendelea kunyakuwa mataji.

Perez alipomuuliza kama anaweza kurejea Madrid mara baada ya timu hiyo kupoteza dhidi ya Ajax, imeonekana kama kitu kisichowezekana kwa Zidane kurejea.

Lakini hata hivyo mapema hii leo siku ya Jumatatu mwandishi wa La Sexta, huku ikidaiwa wakati wowote Zidane huwenda akatangazwa mara baada ya kikao cha bodi.

Zinedine Zidane ameiyongoza Real Madrid kutwaa mataji matatu mfululizo ya Champions League na kisha kuachana na klabu ambayo kwa sasa inanolewa na Solari.Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW