Habari

Mufti wa Tanzania awakanya Diamond, Harmonize na wasanii wengine wanaofuturisha na kucheza nyimbo za kidunia (+video)

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakari Zuberi amewataka waislamu ambao wanawafturisha waislamu wenzao waliofunga kufuata taratibu za dini na kuacha kufanya mambo ambayo yapo kinyume na taratibu.

Ameyasema hayo Jumapili hii katika Mashindano ya Kuhifadhi Quran Tukufu yaliyofanyika Diamond Jubilee ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Katika Iftar ya Harmonize iliyofanyika wiki iliyopita, alifanya show ya kutambulisha wimbo wake mpya wa kidunia ambapo wasanii kadhaa wa WCB akiwemo Diamond Platnumz walipanda jukwaaani na kuibua hisia tofauti kwa waislamu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents