Michezo

Muguruza awapiku Serena na Venus Williams WTA

Mchezaji tenis raia wa Hispania mwanadada, Garbine Muguruza ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka na Chama cha mchezo wa tenis cha wanawake duniani (WTA).

Garbine Muguruza ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka na Chama hicho (WTA) baada ya kuwa namba moja duniani katika viwango vya mchezo huo kwa upande wa wanawake na kumshinda Venus Williams kwa kunyakuwa taji la Wimbledon.

Muguruza mwenye umri wa miaka 24 amekuwa mchezaji wa kwanza kuwashinda mtu na ndugu yake Serena na Venus Williams katika hatua za fainali kama alivyofanya hivyo kwa Serena mwaka 2016 na kutwaa taji la mashindano ya wazi ya Ufaransa (French Open).

Baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa dunia Muguruza ameuambia mtandao wa WTA “Kuwa mchezaji namba moja WTA duniani ni ndoto ambazo zimetimia.” Muguruza ameuambia mtandao huo wa WTA.

Muguruza ameongeza “Kila ilipofika siku yangu ya kuzaliwa huzima mishumaa na kuomba kutimiza ndoto za kuwa mchezaji bora.”

“Nyuma ya hili kuna juhudi kubwa imefanyika mpaka kufikia mafanikio na upendo mkubwa katika mchezo huu lakini pia kipindi kigumu kimepita hadi kufikia kipindi hiki kizuri.”

Muguruza atashuka dimbani wiki ijayo katika fainali za WTA huko Singapore.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents