Burudani

Muigizaji Jason Statham na mpenzi wake wapata mtoto wa kiume

Muigizaji wa filamu kutoka Hollywood ambaye ni raia wa Uingereza, Jason Statham na mpenzi wake Rosie Huntington-Whiteley wamefanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza Jumamosi iliyopita.

Kupitia mtandao wa Instagram, Rosie ameweka picha ikiwa inamuonyesha upande mmoja mtoto wao huyo ambaye wamempa jina la Jack Oscar Statham.

“Our little man arrived! Jack Oscar Statham – 8.8lbs on Saturday June 24th. ??❤️,” ameandika mwanamitindo huyo kwenye picha hiyo hapo juu aliyoiweka kwenye mtandao huo.

Mwezi February ya mwaka huu, Rosie aliweka picha kwenye mtandao huo akionyesha kuwa ni mjamzito. Wawili hao walianza mahusiano tangu mwaka 2010.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents