Bongo Movie

Muigizaji mmoja afa akiigiza Expandable2

Arnold-Schwarzenegger-Sylvester-Stallone-Bruce-Willis-the-expendables

Kwa wale wapenzi wa filamu, husasani za ubeba nadhani sasa wapo kwenye mikakati ya kuisubiri filamu mpya ya Expendable 2, baada ya ile namba moja ilikusanya wakali kibao.




Kama alivyotangaza mkali wa filamu za ubabe Arnold Schwarzenegger, kwamba anarudi tena upya kwenye filamu baada kuchemka vibaya kwenye siasa, sasa ameamua kuingia kwenye filamu upya. Hata hivyo jumatano katika uchukuaji wa filamu huko  Bulgaria umepelekea kupoteza maisha ya muigizaji  anayetumia jina la Stuntman  huku wengine wakipata majaraha.

Ajali hilo ilitokea kilo mile 15, kutoka katika mji wa Sofia katika bwawa la Ognyanovo, katika boat ambayo walikuwa wakiitumia katika shughuli zao.

Mtayarishaji na Muongozaji wa filamu hiyo  Sylvester Stallone ‘Rambo’, yeye hakuwepo kwenye ajaari hiyo kutokana nafasi yake haikuwepo ya kucheza.  Kampuni inayotengeneza filamu hiyo Nu Image/Millennium Films, imewaambiwa polisi kwamba hiyo ni ajali kama ilivyokuwa nyingine, ingawa polisi wamesema wameanza uchunguzaji wa ajari hiyo.

Wakali watakao ng’ara kwenye  filamu hiyo ni  Stallone ‘Rambo’, Arnold Schwarzenegger, Bruce Willis, Dolph Lundgren, Jet Li, Chuck Norris and Jean-Claude Van Damme.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents