Tragedy

Muigizaji wa Bongo Movie Jaji Khamis aka Kashi afariki dunia

Muigizaji wa filamu nchini Jaji Khamis (Kashi) amefariki dunia mchana huu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

936957_207421976072897_1906897483_n

Kashi amewahi kutamba na mchezo wa ITV, Tamu Chungu akiwa na wasanii wenzake kama Mzee Masinde,Samson na wengine.

Baada ya kupata habari hii, Bongo5 imeongea na muigizaji mwenzake Monalisa ambae amethibitisha kutokea kwa msiba huo. Monalisa amesema alipata taarifa jana kwamba Kashi amelazwa hospitali akiwa amezidiwa kiasi cha kushindwa kuongea na hivyo kushindwa kujua nini kilikuwa kinamsumbua.

Naye Hemedy PHD ametweet: REST IN PEACE MUIGIZAJI MWENZETU JAJI KHAMIS KASHI….MUNGU AKULAZE PEMA PEPONI…MOVIE YA MWISHO TULICHEZA WOTE ILIKUA MATILDA!!Sad newz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents