Burudani

Muigizaji wa filamu ya ‘Captain Phillips’ msomali ‘Barkhad Abdi’ adaiwa kupigika (broke)

Matarajio ya wengi ni kuwa Barkhad Abdi aliyeigiza kama haramia kwenye filamu ya Captain Phillips ni milionea kwa sasa. Well, si kweli. Msomali huyo anadaiwa kupigika tayari.

HARG9780

Muigizaji huyo aliyetajwa kuwania tuzo za Oscar mwaka huu alilipwa dola 65,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 100 na sasa hivi akaunti yake inasoma zero.

HARG9644v2

Awali Barkhad Abdi alikuwa akifanya kazi kwenye duka la simu la kaka yake na pia amewahi kuwa dereva wa limousine kabla ya kwenda kwenye usaili wa filamu hiyo. Kuna taarifa kuwa kampuni iliyoandaa filamu hiyo ndio inayomsaidia kwa sasa kwa kumlipa hela ya malazi kwenye hoteli ya Beverly Hilton jijini Los Angeles na kwamba nguo alizovaa kwenye tuzo za Oscar ni za kukopa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents