Burudani

Muigizaji wa filamu za James Bond afariki dunia

Muigizaji Clifton James, maarufu kama ‘JW Pepper’ kwenye filamu mbili za James Bond, amefariki dunia akiwa na miaka 96.

Alifariki karibu na mji wa Gladstone, Oregon, siku ya Jumamosi kutokana na matatizo ya ugonjwa wa kisukari.

James alifahamika sana kutokana na uigizaji wake katika filamu za Bond za ‘Live and Let Die’ na ‘The Man with the Golden Gun’ miaka ya sabini.

Binti yake Lynn amesema: ”Alikuwa mtu mpenda watu na mwenye uwazi sana. Alipendwa sana na kila mtu.”

Aliongeza: “Sidhani alikuwa na adui hata mmoja. Kwa kweli tulibarikiwa kuwa na yeye maishani.”

Sir Roger ameandika: “Nasikitika sana kusikia Clifton James ametuacha. Kama JW Pepper aliboresha sana na kuongeza ucheshi katika filamu zangu mbili za kwanza za James Bond.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents