Tragedy

Muimbaji wa Chamber Squad Mez B afariki dunia

Muimbaji wa kundi la Chamber Squad, Maze B, amefariki leo saa nne asubuhi, kwa mujibu wa mtu aliyekuwa akimuuguza. Msanii huyo aliyewahi kufanya vyema na wimbo wake ‘Fikiria’ alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Mwananchi mjini Dodoma.

1208344_1539903592937807_1437246943_n

Mez B aliyezaliwa kwa jina la Moses Bushagama alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Pneumonia.

Hivi karibuni aliongea na E-News ya EATV na alikuwa anaendelea vyema:

“Nilikuwa na tatizo la Pneumonia tokea mwezi wa 12 nikawa nipo vizuri nilivyo kuja tena Dodoma hali ikabadilika ndo nipo hospitali nimelazwa nasumbuliwa na maumivu ya kichwa na shingo,” alisema.

“Nategemea kuruhusiwa muda wowote na sasa hivi naendelea vizuri.”

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents