Burudani

Muimbaji wa Kenya Otile Brown aingia kwenye mvutano na lebo yake

Kimya kimya inaonekana kama kuna vita baridi kati ya msanii wa muziki wa kizazi cha sasa, Otile Brown na lebo ya Dreamland Music Empire inayomilikiwa na Dr.Eddie.

Itakumbukwa kwamba Otile Brown alitambulishwa rasmi kwenye game ya muziki na Dr.Eddie ambaye ndo aliyetayarisha audio pamoja na video ya wimbo ‘Romeo na Julie’ aliyomshirikisha rapper Khaligraph Jones. Kutokea hapo msanii huyu amekuwa akiachilia hit songs zikifuatana.

Inasemekana kuna vuta nikuvute za hapa na pale kati ya muimbaji huyu ambaye pia ana uwezo wa kurap na Dr.Eddie. Kuthibitisha kwamba kuna kitu kinachoendelea, niligundua kwamba mizigo yake imeshaondolewa youtube. Katika mahojiano na Juma Balo kwenye runinga ya K24 (Kenya), Otile alisema haya:

“Okay Dr.Eddie namheshimu sana, ni mtu ambaye mpaka hapa nilipofika ana mchango mkubwa sana kwenye muziki wangu, na tumetoana mbali katika hii biashara ya muziki. Kwahiyo inaweza kufika wakati unahisi mambo hayaendi kama yanavyofaa, so unajikuta mnaanza kukwaruzana kwa njia moja au nyingine na katika biashara issue kama hizo zinatokeaga.”

Aliendelea, “But I respect him kwa sababu ana mchango mkubwa sana katika muziki wangu. So it’s not a big issue tutaimaliza soon halafu kila kitu kitakuwa sawa. Naomba tu tuzidi kutoa support.”

Nahisi kwamba kuna mzozo unaoendelea japo Otile hakuongea kwa upana zaidi kuhusu suala hilo.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Niseme Nawe’ aliomshirikisha Barakah da Prince, ameahidi kuachia kazi mbichi soon.

By:Teddyza Agwa
Instagram @teddyzabway
+254710487436

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents