BurudaniVideos

Muimbaji wa Longombas, Lovy kushiriki kutayarisha soundtrack ya Fast and Furious

Producer na member wa kundi la Longombas la Kenya, Lovy, amepata shavu la kutayarisha soundtrack ya filamu ya Fast and Furious 8, itakayotoka April 14, 2017.

Filamu hiyo inahusisha mastaa kama Vin Diesel, Michelle Rodriguez, Dwayne Johnson, Tyrese Gibson, Ludacris, Charlize Theron na wengine. Lovy ameitoboa habari hiyo njema wakati akizungumza na Willy M Tuva nchini Marekani.

“Ntasema I am making a lot of money, I am climbing the ladder 2014 nilipata Grammy nomination yangu ya kwanza kufanya kazi na Iggy Azalea. Nimewafanya kazi na karibu kila mtu, nilikuwa nimekaa hapa umeona simu yangu ikiita naambiwa niende nifanye Fast and Furious,” amesema Lovy.

Kwa upande mwingine Lovy amesema haikuwa rahisi kuondoka Kenya wakiwa kwenye kilele cha mafanikio na kwenda kuanza upya Marekani ambako wana miaka 9 sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents