Habari

Multichoice Group kutoa zaidi ya Sh Bilioni 10 kusaidia wazalishaji wa maudhui wakati wa Janga la COVID-19 

Wakati hali ya janga la ugonjwa wa virusi vya Corona (Covid-19) likiendelea kuitikisa dunia, Kampuni ya MultiChoice imetangaza mpango wake wa kutoa randi milioni 80 (sawa na takriban shilingi bilioni 10.5) kusaidia wazalishaji wa maudhui katika kipindi hiki cha kupambana na virushi vya Corona.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Afisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya MultiChoice Calvo Mawela amesema “dhamira yetu ni kuhakikisha watu wote wanaofanya uzalishaji wa maudhui yetu kote barani Afrika wanaendelea kupata kipato chao bila kuathirika katika wakati huu. Tunataka wadau wetu hawa muhimu wasiathiriwe vibaya na hali ya sasa ambapo kazi nyingi za uazalishaji zimesimama.

Taarifa hiyo pia imebainisha kuwa kwa kupitia programu yake ya MultiChoice Talent Factory (MTF) kampuni hiyo itazindua ulingo wa mafunzo maalum kwa njia ya mtandao (online learning portal) itakayowezesha zaidi ya watu 40,000 wa tasnia ya uzalishaji maudhui kupata mafunzo ya kawaida na mafunzo maalum (master classes). Mafunzo haya yatawafanya wana tasnia waendelee kujifunza huku wakizingatia maagizo ya mamlaka za afya yanayowataka watu kuepuka mikusanyiko na kukaa nyumbani katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona.

Kwa sasa kila sekta kote ulimwenguni imekuwa ikipitia kipindi cha mabadiliko na changamoto nyingi zinazotokana na maradhi haya na kwakuwa MultiChoice ni mdau mkubwa katika sekta ya habari na burudani nayo  imeamua kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa inasimama na wadau wake pamoja hata katika nyakati ngumu kama hizi

Kote barani Afrika, shughuli za uzalishaji wa maudhui zimeathirika sana huku nchi nyingine zikiwa tayari zimesitisha shughuli hizo kwa muda. Hii imesababisha MultiChoice kuamua kutekeleza hatua mbalimbali zenye lengo la kulinda maslahi  na vipato vya wazalishaji pamoja na ustawi mzima wa kampuni za uzalishaji maudhui. MultiChoice inaamini kuwa hatua hizi zinazochukuliwa zitatia chachu katika sekta ya uzalishaji maudhui katika kipindi hiki kigumu.

Sekta hii ya uzalishaji maudhui inaajiri maelfu ya watu wakiwemo waigizaji, wapiga picha, wabunifu na wengineo. Watu wote hawa ni muhimu sana na ndiyo nguzo ya kuhakikisha watazamaji wa vipindi na jamii kwa ujumla wanapata elimu, burudani, na habari.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents