Michezo

MultiChoice yaanzisha channel ya saa 24 itakayorusha kesi ya Oscar Pistorius

Kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha wa nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius itakuwa na channel ya saa 24.

article-2278492-179495C4000005DC-157_634x906
Oscar Pistorius na mpenzi wake aliyemuua, marehemu Reeva Steenkamp

MultiChoice ambao ni wasambazaji wakuu wa runinga za cable nchini Afrika Kusini, wamesema Jumatano hii. Kampuni hiyo imesema channel hiyo ya muda itazinduliwa March 2, siku moja kabla ya kesi ya mwanariadha huyo mlemavu kuanza kusikilizwa kwenye mahakamu kuu jijini Pretoria kufuatia kumuua mpenzi wake nyumbani kwake katika Valentine’s Day mwaka jana.

Pistorius alimuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi kupitia mlango wa choo, Feb. 14. Alisema alidhania Steenkamp alikuwa mvamizi na hivyo kumpiga risasi kujilinda japo waendesha mashtaka wanadai kuwa wawili hao walikuwa na mabishano kabla na hivyo Pistorius alimuua msichana huyo kwa kudhamiria kutokana na hasira.

Channel hiyo ya runinga imepewa jina “The Oscar Pistorius Trial: A Carte Blanche Channel,” na itakuwa ikiendeshwa na watayarishaji wa kipindi cha habari za uchunguzi cha Afrika Kusini, Carte Blanche,” ambacho huoneshwa kwenye DSTV.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents