Habari

Mume amkata shingo jirani

Ama kweli mke wa mtu ni sumu kali ambayo kuichezea ni kujihatarishia maisha kama ilivyokuwa kwa bwana mmoja aliyeuawa baada ya kubambwa laivu akijivinjari na mke wa mtu.

Na Stephen Wang�nyi, PST – Shinyanga



Ama kweli mke wa mtu ni sumu kali ambayo kuichezea ni kujihatarishia maisha kama ilivyokuwa kwa bwana mmoja aliyeuawa baada ya kubambwa laivu akijivinjari na mke wa mtu.


Mwanaume huyo aliyeuawa kwa kuvunjwa shingo ametajwa kwa jina la Kazimili John, 28, mkazi wa kijiji cha Mwanese wilayani Kahama.


Akizungumza na mwandishi wa PST, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Isuto Mantage, amesema tukio hilo la kinyama lilitokea hivi karibuni.


Amesema mwanamume huyo anadaiwa kuuawa na mtuhumiwa aitwaye Robert Jiganze, 25, ambaye ni mume wa mwanamke anayedaiwa kukutwa akifanya mapenzi na marehemu.


Kwa mujibu wa Kamanda Mantage, marehemu alikuwa akiishi jirani na wana ndoa hao na kwamba siku ya tukio majira ya saa 6:00 mchana, mume wa mwanamke huyo alipofika kwake, alishtuka kukuta wawili hao wakiendelea kupeana raha.


Akasema kwa hasira alimvamia mgoni wake na mara purukushani zikafumka. Akasema aliendelea kumuadhibu mgoni wake huku akiwa kama alivyozaliwa.


“Mwisho wa purukushani hizo, Bw. Jiganze aliweza kumvunja vunja shingo mgoni wake John na kumuua,“ akasema Kamanda.


Kaimu Kamanda Mantage amesema baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alitiwa mbaroni.


Wakati huohuo, Kaimu Kamanda Mantage amesema jeshi lake linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata shingo kwa panga marehemu Sospeter Bosco ,23, mkazi wa kijiji cha Kabale wilayani Bariadi mkoani hapa.


Kaimu Kamanda Mantage amesema tukio hilo la kinyama lilijiri wiki iliyopita mishale ya saa 7:00 mchana.


Amesema tukio hilo la mauaji lilifanyika mbele ya mke wa marehemu.
Kwa mujibu wa Kamanda Mantage, hadi sasa watu wanne wanatuhumiwa kuhusika na mauaji hayo, wakiwemo wakazi wawili wa kijiji cha Kabale.


Souce: Alasiri

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents