Tia Kitu. Pata Vituuz!

Mume na mke kutoka China wahukumia kutoa faini kwa kumhongo kamishina wa TRA DSM – Video

Mume na mke kutoka China wahukumia kutoa faini kwa kumhongo kamishina wa TRA DSM - Video

Siku ya leo februari 26 ilmetolewa hukumu kwa raia wawili kutoka nchini China ambao ni Zheng Rongman(50) na Mkewe Ou Ya(47), katika Mahakama ya Kisutu, kulipa faini Tsh. Milioni moja kila mmoja kwa kukiri kutoa rushwa ya USD 5000 ambazo ni sawa na (Tsh 11.5 M) kwa Kamishna Mkuu TRA Dkt Edwin Mhede, Mambazo zitakuwa ni mali ya Serikali.

Wawili hao wamehukumiwa kulipa faini na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Huruma Shaidi. Ambao mnamo February 24, 2020, washtakiwa hao walifika Makao Makuu ya TRA, DSM kuonana na Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Edwin Mhede na kulalamika kuwa wamekadiriwa kiwango kikubwa cha kodi. Imeelezwa kuwa Walimkabidhi Kamishna huyo USD 5000 (Tsh. 11.5 M) hongo ili awape msaada katika suala lao la kodi, ambayo mwanzo walitakiwa kulipa kodi ya Tsh. Billion 1.3.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW