DStv Inogilee!

Mume wa mwanamuziki Celine Dion afariki dunia

Rene Angelil, mume wa mwanamuziki mashuhuri duniani Celine Dion, amefariki dunia siku ya Alhamisi (Jan 14) huko nyumbani kwao Las Vegas baada ya kuugua saratani, mwanamuziki huyo ametangaza.

celin na mumewe

Bw Angelil, aliyemuoa Dion mwaka 1994 na wakajaliwa kupata watoto watatu, amekuwa pia akifanya kazi kama meneja wa mwanamuziki huyo mkongwe.

Dion alichukua likizo kutoka kwenye muziki kwa vipindi viwili ili kumuuguza Angelil baada ya kupatikana na saratani ya koo mwaka 2000.

Bw Angelil alizaliwa mjini Montreal mwaka 1942 na amefariki akiwa na miaka 73.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW