Muonekano wa Wema Sepetu wazua gumzo mitandaoni, Mashabiki wamuandama na kumwambia maneno haya – Video

Muonekano wa Wema Sepetu wazua gumzo mitandaoni, Mashabiki wamuandama na kumwambia maneno haya - Video

Msanii wa filamu na Miss Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu, amezua gumzo mitandaoni baada ya kupost picha kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha mwili wake kuonekana kuzidi kupungua, Wema Sepetu ambae aliamua kupunguza mwili wake kwa madai ya kuwa unamnyima raha hasa katika kazi zake za kisanaa.

Ikumbukwe kuwa katika mahojiano aliyoyafanya kupita App yake ya Wemapp alisema, ameamua kupunguza mwili wake kwa sababu ulikua unamletea shida sana hasa kwa upande wa filamu kuna mavazi alikua hawezi kuyavaa na kuna baadhi ya Scenes zilikuwa zinampa shida kuigiza kulingana na mwili aliokuwa nao kipindi cha mwanzo

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema aliamua kupost picha akiwa na wadada wengine wawili akiambatanisha na ujumbe kuwa “Alhamdulillah Rest Easy kaka” picha hii ilimuonyesha akiwa ametoka kwenye msiba wa kaka ake anaeitwa Mkusa Sepetu, ambaye alikuwa Jaji wa Mahakama kuu Zanzibar ambaye alipoteza maisha asubuhi ya Feb 16, 2020.

View this post on Instagram

Alhamdulillah…❣️ . . . Rest Easy Kaka…

A post shared by Wema App (@wemasepetu) on

Wema baada ya kupost picha hiyo mashabiki wake wakaanza kumuandama kwa maneno mengi huku wakimwambia ameathirika, wengine wakamuambia ajitahidi kula maana wakikutana nae barabarani wanaweza kumsahau kabisa kutokana na mwili wake unavyozidi kuisha. Baada ya comment za mashabiki kuzidi Wema hakukaa kimya aliamua kuwajibu na kuwaambia kuwa Ni kweli ameathirika na kama watamsahau basi yeye ndivyo anavyotaka.

By Angel Mmasi.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW