Siasa

Museveni atetea kufunga mitandao ya kijamii kabla ya uchaguzi (+ Video)

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amethibitisha kuagiza mitandao kadhaa ya kijamii nchini humo kufungiwa.

Katika hotuba yake iliyooneshwa mubashara katika televisheni usiku wa Jumanne saa tatu kabla ya muda wa mwisho wa kufanya kampeni, Rais Museveni aliyekuwa amevalia koti la kijeshi alisema ameagiza kufungwa kwa mtandao wa kijamii wa Facebook kwa kuwa na kiburi na kupendelea upande mmoja.

Alisema ikiwa Facebook itatumiwa nchini Uganda, lazima itumiwe kwa usawa na kila mtu anayetaka kufanya hivyo. Bw. Museveni pia alisema hatakubali mtu yeyote kucheza na nchi yake ama kuamua ni nani mzuri au mbaya.

Hatua ya Rais inakuja siku moja baada ya Facebook kuthibitisha kwamba imezifungia akaunti zinazohusishwa na serikali ikidai kuwa zinatumiwa kushawishi mijadala ya umma katika kinyang’anyiro kikali cha uchaguzi, ambapo rais aliye madarakani na mpinzani wake mkuu, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine wanatafuta ushindi wa kura za vijana.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii ya Facebook na WhatsApp, Instagram na Snapchat walianza kulalamikia kukatizwa kwa huduma hizo mapema siku ya Jumanne.

Twitter imejibu hatua hiyo ikisema kuzingiwa kwa huduma za intaneti ni hatari na inakiuka haki za kimsingi za binadamu na kanuni ya uhuru wa mawasiliano.

Wakati huo huo Marekani imelaani uamuzi wa serikali kufunga mitandao ya kijamii, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akitoa wito wa kuheshimiwa haki za binadamu.

Bofya hapa chini;

https://www.instagram.com/tv/CJ-riPIBItz/

https://www.instagram.com/tv/CJ-riPIBItz/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents