DStv Inogilee!

Museveni, Kagame na Mugabe walijisikiaje kuhudhuria Magufuli akiapishwa?

Watu wengi tumekuwa tukifikiri kwamba kwanini Marais hawa hawaoni aibu pale ambapo wenzao wanaoingia madarakani na kuondoka wao wakiwa wamebakia palepale kwenye hayo madaraka?

_86532078_0a3754dc-e05a-477f-a135-1541670339ca

Inawezekana wamekuwa wanafunzi ambao hawawezi kuelewa somo wakidhani ya kuwa wao ni marais wa kudumu kwenye nchi zao. Kitu kingine ambacho inawezekana hawaelewi kwanini Tanzania marais wanaondoka madarakani bila kuwa ving’anga’nizi kama wao?

Viongozi hawa wameshindwa kutengeneza mfumo wa kuwawezesha wengine kuweza kushika nafasi hiyo, hivyo kimewafanya wakose imani kama wengine wanaweza kuongoza badala ya wao.

Kiongozi bora huwaandaa watu wengine waweze kuongoza nyadhifa walizonazo na hii huongeza uwezo wa taaasisi kuwa imara hata kiongozi huyo mkubwa anapoondoka.

Uongozi wa kuwajengea uwezo wa kuongoza unadhihirika wazi kwenye mashirika ambayo huwa hayategemei mtu mmoja tu kama kiongozi bali wanakuwa wamewawezesha wengine kuweza kuongoza au kushika madaraka hayo makubwa bila kutetereka.

Yoweri Museveni wa Uganda anawania awamu ya tano katika nchi hiyo anayoiendesha kibabe huku kukiwa hakuna dalili ya yeye kuachia madaraka hivi karibuni. Kuonyesha kwamba bado ana nguvu za kuongoza, alionyesha mfano kwa kukimbia mbio huku walinzi wake wakitamtazama.

Huu ni wakati wa bosi huyu wa Uganda kuachia ngazi na kuruhusu watu wengine wachukue madaraka. Rais Museveni anachojaribu ni kuvuta muda ili akizeeka kabisa aweze kuweka mtu anayefikiri ndiye atakayeiongoza Uganda kama anavyotaka kitu ambacho anaweza asifanikiwe na vilevile kinaweza kusababisha machafuko zaidi katika nchi hiyo mara tu atakapoondoka kwani kila mtu ataanza kuangalia namna gani na yeye aingie madarakani.

President of Uganda Yoweri Museveni attends the Clinton Global Initiative on September 26, 2013 in New York. AFP PHOTO/Mehdi Taamallah (Photo credit should read MEHDI TAAMALLAH/AFP/Getty Images)

Paul Kagame, kwake yeye anajiona ni mkombozi ambaye anahitajika na nchi yake hivyo na yeye alilazimika kubadilisha katiba aweze kuongeza kipindi kingine madarakani. Swali je ataongoza milele na kama kuna siku ataondoka amejipanga vipi? Hawakusikia kwamba Rais Kikwete alisema miaka kumi kwa Urais inatosha kabisa kufanya ulichotakiwa kukifanya?

Ingawa Tanzania inaongozwa na chama kimoja mpaka sasa lakini ndani ya chama kuna demokrasia ya kuruhusu madaraka kuhama kutoka kwa kiongozi mmoja kwenda mwingine. Sijaelewa wao wanashindwaje hata kuanza na hilo kwanza kabla ya kuelekea kwenye kiwango kingine cha demokrasia.

Jambo hili la kung’ang’ania madaraka linatengeneza bomu ambalo mwisho wa siku huwa halizimiki kirahisi. Mwalimu Nyerere aliligundua hilo mapema akaamua kung’atuka kwenye nyadhifa hiyo nyeti ambayo Marais wa bara ya Afrika imekuwa ngumu sana kuondoka kwenye kiti hicho kirahisi.

president-paul-kagame-7

Robert Mugabe, inawezekana ndiye rais anayejulikana kwamba ni mzalendo wa nchi yake ingawa anaishi maisha ya kifahari zaidi na ni mzee sana huku hataki kuachia madaraka katika nchi hiyo.

Rais Mugabe aliyeliongoza taifa hilo tokea lipate uhuru wake mpaka sasa bado anaendelea ingawa kumekuwa na matukio ya kudondoka mara kadhaa kutokana na afya kuzorota  pamoja na umri  mkubwa alionao.

Ingawa watafiti wa karibu wa mwenendo wa nchi hiyo wanadai inawezekana mkewe, Grace anaweza kuongoza nchi hiyo baada ya Mugabe kuondoka kutokana na ushawishi alionao kwenye jeshi la nchi hiyo.

Grace Mugabe anadaiwa kuwa na tabia za kidikteta.

Hata hivyo wengine wanampa nafasi aliyewahi kuwa makamu wake wa Rais Joyce Mujuru kwani hata yeye ana ushawishi mkubwa kwenye jeshi la nchi hiyo zaidi ya Grace na makamu wa rais wa sasa Emmerson Mnangagwa.

_86532270_9f1cc529-b594-49a1-9573-34f98b8b63e1

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW