Siasa

Music Addiction: Rais Obama amchanganya kansela wa Uingereza ‘George Osborne’ kwa kumuita mara 3 jina la star wa R&B wakati wa hotuba

Rais wa Marekani Barrack Obama ambaye anayetarajiwa kuanza ziara barani Afrika hivi karibuni , Jumanne wiki hii (June 18) wakati akitoa hutuba katika mkutano wa nchi tajiri zaidi duniani G8 huko Ireland kaskazini, alijikuta akimchanganya ‘Chancellor of the Exchequer’ wa Uingereza George Osborne kwa kumuita (Jeffrey) jina la mwanamuziki wa R&B ambaye naye anaitwa Jeffrey Osborne.

osbornes
Kushoto ni Kansela George Osborne / Kulia ni star wa R&B Jeffrey Osborne

Kukosea kwa Obama kulitokana na sababu kama mbili hivi ya kwanza ikiwa ni mfanano wa majina ya mwisho ‘Osborne’ , lakini sababu ambayo inaonekana kuwa kubwa zaidi ambayo hata yeye (Obama) ali admit ni kuwa Jeffrey ni favorite R&B singer wake.

Kwa mujibu wa Sky News baada ya Obama kugundua kuwa alikuwa anamchanganya George na Jeffrey alimuomba radhi George , “I’m sorry, man. I must have confused you with my favourite R and B singer,”.

Pamoja na kwamba Obama alimchanganya bwana George na Jeffrey kwa bahati mbaya, lakini ilikuwa ni habari njema kwa mwanamuziki huyo wa R&B mmarekani mweusi mwenye miaka 65, ambaye baada ya kuhojiwa alisema kuwa amefurahi kwasababu hakujua kama Obama ni shabiki wake mkubwa kiasi cha mpaka kumwita Kansela George ‘Jeffrey’ Osborne.

“I was really delighted actually. I was really not aware that (Obama) was that much of a fan that he would call the chancellor Jeffrey Osborne” alisema Jefrrey.

Msikilize Jeffrey

http://youtu.be/KXVe7zUPGms

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents