Tia Kitu. Pata Vituuz!

MUSIC AUDIO: Diamond aachia ngoma yake mpya ya ‘BABA LAO’. Je, ni kweli ame-copy na ku-paste ngoma ya ‘Soapy’ ya Naira Marley?

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameachia wimbo wake mpya wa ‘BABA LAO’, Wimbo ambao umegonga vichwa vya habari hapa Tanzania kutokana na aina ya uchezaji wake.

Wimbo huo umeanza kuchukua headlines nchini Nigeria ambapo baadhi ya mashabiki wanaufanisha na wimbo wa SOAPY wa msanii anayekuja kwa kasi nchini humo, Naira Marley.

Wimbo wa SOAPY una miezi miwili tu tangu uachiwe lakini nchini Nigeria umeanza kusikika sana kwenye Media kutokana na lugha na melody aliyoitumia Naira Marley.

Je, Kwa kusikiliza ni kweli Diamond ame-copy wimbo wa kijana huyo Naira Marley? Kumbuka mdundo wa ngoma hiyo umegongwa na S2kizzy na Lizer Classic.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW