BurudaniHabariVideos

Music Video Zapigwa Marufuku

Darda KingBaadhi ya Video za muziki ambazo hivi karibuni zimezua sokomoko kwenye vituo vya televisheni, zimefungiwa kuonyeshwa.

Darda KingNa Sulemani.

Baadhi ya Video za muziki ambazo hivi karibuni zimezua sokomoko kwenye vituo vya televisheni, zimefungiwa kuonyeshwa. Mojawapo ya video hizo iliyoleta mtafaruku zaidi ni video ya ‘Yihoo’ ya msanii wa miondoko ya bongoflava Darda King. Video hiyo kabla ya kufungiwa kuonyeshwa ilikuwa ikijadiliwa na waendesha vipindi vya televisheni mbalimbali. Kulingana na mtazamo wa mwendesha kipindi cha Planet Bongo cha EATV Salama, video hii imeonyesha asilimia fulani ya udhalilishaji wa mwanamke.

Udhalilishaji wa mwanamke ama matumizi mabaya ya mwanamke kwenye video za muziki imekuwa ni kero kubwa kwa watazamaji wa Afrika Mashariki, watazamaji wengi wamekuwa wakilalamika wakidai video zenye kudhalilisha ama kuwashusha hadhi wanawake zisionyeshwe huku wachache wakisema hiyo ni mojawapo ya burudani. Hapo awali mtafaruku huu ulikuwa kwenye video za miziki ya kikongo ambazo nyingi zilikuwa zikionyesha wanawake wakicheza nusu uchi, siku za usoni staili hiyo imekuwa ikihamia kwenye miondoko ya bongoflava taratibu.
Kabla ya kufungiwa video ya Darda King ilikuwa ni video namba moja kwa wiki tatu mfululizo kwenye chati za Afrika Mashariki, hii inaonyesha kwa kiasi fulani labda watazamaji wanavutiwa zaidi na video zinazodhalilisha wanawake.

Wakizungumzia suala hili waandaa vipindi vya televisheni wamewaomba wanamuziki na waandaa video kuwa wabunifu zaidi katika utengenezaji wa video hizi bila kudhalilisha wanawake.

Source: Bongo5

{mos_sb_discuss:6}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents