Bongo Movie

Mussa Banzi kuja na filamu mpya ‘Gawa’

Mtayarishaji na muigizaji wa filamu nchini Mussa Banzi anatarajia kuingiza sokoni kazi mpya iliyopewa jina ‘Gawa’.
Filamu hiyo itakuwa inaelezea maisha ya kijijini ambapo Mussa na mwanadada Husna Chobiss ni wahusika wakuu.

FILAMU-YA-GAWA-SIZE

Musa ambaye anasifika kwa utunzi wa miswada mingi ya filamu nchini amesema ameamua kuigiza kwenye Gawa ili kuendelea kuonesha uwezo wake katika upande wa uigizaji.

“Kazi yangu kama muongozaji ni kuhakikisha ninapoandika au kupewa hadithi ninamtafuta msanii anayevaa uhusika, na kama hajafikia kiwango hicho basi ni wajibu wangu pia kumjenga ili aweze kufikia kiwango cha uigizaji lakini jambo tunalokutana nalo ni wasanii kujisahau, hivyo kwa kuona hivyo nimeingia rasmi kuigiza na uwezo wangu ni katika filamu ya Gawa,” amesema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents