Habari

Mustafa Hassanali aalikwa kwenye Maonyesho ya color in the Desert

Mwanamitindo mkongwe ndani ya Afrika anayetokea Tanzania Mustafa Hassanali amealikwa katika maonesho ya mitindo ya color in the desert yanayoanza kufanyika kuanzia leo tarehe 31 Agost hadi tarehe 1 Septemba ikiwa ni mara ya pili kufanyika nchini Botswana katika mji mkuu wa Gaborone.
Mustafa ni mtanzania pekee aliyealikwa katika maonesho hayo ya mavazi yanayosifika Barani Afrika, na kwa ujumla Hassanali amesema “ Nimefurahi sana na anajisikia fahari na heshima kuzindua toleo langu jipya la mtindo ikiwa ni la nne ndani ya mwaka huu na nategemea kutumia fursa hii kuutangaza utamaduni wetu na kuboresha urafiki uliopo kati ya Botswana na Tanzania”.

Aidha Mustafa alisema katika onyesho hili linaloitwa Pink Desert collection yeye atawakilisha magauni yenye alama zenye nembo zake mpya ikiwa ni pamoja na nguo za kiume ambazo ziko tayari kwa kuvaliwa na kuonesha umaridadi wa mbunifu huyo.

Akimalizia Mustafa alisema “Nitatumia toleo hili la mitindo pia katika kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusiana na tatizo la ugonjwa wa kansa ya matiti ili kila mwanamke aweze kuwa na uelewa wa kujichunguza mwenyewe juu ya afya yake, sambamba na kupenda kuvaa nguo zenye rangi ya pinki kama kiashiria cha uelewa juu ya kansa ya matiti ugonjwa ambao unaathiri wanawake wengi”.

Kwa mwaka 2012 Mustafa Hassanali ameshazindua matoleo matatu ya mavazi ambayo ni, Afrikalos aliyoonesha Nchini Nigeria (Lagos), Toleo la Harusi aliloonesha Tanzania (Dar es salaam) na toleo maalumu la mwezi wa Ramadhani liliooneshwa Dakar Senegal.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents