Mitindo

Mustafa Hassanali kuipeleka Swahili Fashion Week Nairobi


Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania, Mustafa Hassanali anatarajiwa kuipeleka Swahili Fashion week kwa mara ya kwanza jijini Nairobi, Kenya.

Hassanali na waandaji wa tukio zima wameahidi masuprise ya nguvu kwa wageni na wabunifu wa mavazi kwenye awamu hiyo ya tano ya Swahili Fashion.

Tukio hilo la fashion litafanyika kwenye ukumbi wa Michael Joseph Centre jijini Nairobi kuanzia October 6.

“This being the first time that the event will be taking place in Kenya we will be looking forward to doing something that will leave Kenyans craving for a second one,” Mustafa aliliambia gazeti la The Star la Kenya.

Swahili Fashion ilianzishwa mwaka 2008 kwa malengo ya kuwapa nafasi wabunifu wa mavazi wa Afrika Mashariki na kati, jukwaa la kuonesha ubunifu na ujuzi wao katika mitindo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents