Habari

Muswada wa sheria ya Ndoa (2013) wazua mjadala Kenya, watakaoshindwa kutimiza ahadi za ndoa matatani

Wiki hii moja ya vitu vilivyozua mijadala mikubwa nchini Kenya ni pamoja na muswaada wa sheria ya ndoa ‘Marriage Bill 2013’ iliyowasilishwa katika bunge la Kenya Jumanne (July 16) ambayo pamoja na mambo mengine, unasema adhabu ya kifungo cha miaka 5 na fidia ya million 1 ya Kenya (zaidi ya m 18TSH) kwa mwanaume/mwanamke atakayetoa ahadi za ndoa na kushindwa kuzitimiza kwa mujibu wa mtandao wa Niaje.

rings

Haya ni baadhi ya mapendekezo yaliyomo katika muswaada huo wa sheria ya ndoa 2013 kwa mujibu wa mtandao wa Ghalfa:

1.Wapenzi ambao wataahidiana ndoa na baadaye mmoja kushindwa kutimiza ahadi hiyo atatakiwa kulipa fidia endapo sheria hiyo itapitishwa.

2.Muswaada huo unatoa nafasi kwa wapenzi kusajili ndoa yao kama ‘monogamous’ inayoruhusu wanandoa kuwa na mume/mke mmoja tu.

3.Endapo mwanaume akitaka kuongeza mke/wake wengine ni lazima mke/wake zake waidhinishe maamuzi hayo, mwanaume ambaye ataoa wake zaidi kwa siri anaweza kushitakiwa

4. Wanandoa watakuwa na haki sawa juu ya mali za ndoa, endapo wanandoa watakubaliana mwanaume aoe wake wengine, haki za mali za ndoa kwa mke wa kwanza zitalindwa.

Muswaada huu umepokelewa kwa hisia tofauti na wakenya ambao wengi wao hususani wanaume wameonesha kutoridhishwa kwa madai kuwa imependelea zaidi upande mmoja wa wanawake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents