Habari

Muuaji katika uzinduzi wa filamu ya Batman aendelea kujifanya ‘Joker’ jela


Uhakika wa kwamba James Holmes, aliyeua watu 12 na kujeruhi wengine zaidi ya 50 huko Denver, Colorado nchini Marekani kuwa ni chizi, unazidi kuongezeka baada ya kuendelea kufanya vituko jela.
Inasemekana kuwa kijana huyo bado anaendelea kujifanya yeye ni Joker kama ilivyo kwenye filamu ya Batman.
Pia baadhi ya wafungwa kwenye gereza la Arapahoe Detention Centre, Colorado, wanakisia kuwa Holmes anaweza kuuawa akiwa jela.
Mara ya kwanza Holmes, 24, aliwaambia polisi kuwa yeye ni Joker adui mkubwa wa Batman baada ya kufanya ukatili huo dhidi ya wananchi wasio na hatia kwenye jumba la kuoneshea sinema.
Tabia yake ya ‘uchizi’ imeendelea gerezani humo hadi kufikia hatua ya kuwatemea mate askari jela.
Mfanyakazi mmoja wa gerezani humo ameliambia gazeti la The Sun kuwa muuaji huyo ambaye yupo chini ya uangalizi mkali ili asijiue kuwa: “Hajaonesha wasiwasi wowote.Yeye anavyodhani ni kama vile anaigiza filamu.”
Mfungwa Wayne Medley, 24 ambaye alikuwa gerezani wakati Holmes anapelekwa alisema: “Wafungwa wote wanazungumza kuhusu kumuua. Kila mmoja alikuwa anatafuta nafasi. Ndicho kitu pekee walichokuwa wakiongelea.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents