Shinda na SIM Account

Muuaji wa kukumbukwa Marekani afariki dunia

Muuaji ambaye hawezi kusahaulika nchini Marekani, Charles Manson amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83.

Manson ambaye alikuwa anatumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa la kuua watu saba na mtoto mmoja ambaye hakuwa amezaliwa huko Los Angeles Marekani mwaka 1969 amedaiwa kufariki siku ya jana (Jumapili).

Akiongea na mtandao wa TMZ, Debra Tate ambaye ni ndugu wa marehemu Sharon Tate aliyekuwa muigizaji maarufu wa Marekani na kuuawa na Manson, amethibitisha kupokea simu kutoka gerezani kuwa muuaji huyo aliyehukumiwa mwaka 1971, amefariki dunia katika hospitali ya Bakersfield


Picha ya Charles Manson akiwa Mahakamani mwaka 1970

Novemba ya mwaka 2014 shirika la habari la Associated Press, liliripoti kuwaManson ameruhusiwa kumuoa mchumba wake Afton Elaine Burton akiwa gerezani.

Mwaka 2012, Manson alinyimwa msamaha wa kuachiliwa (Parole) na jopo la gereza la mjini California, hiyo ilikuwa ni mara ya 12 kwake kuomba kuachiliwa huru.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW