Shinda na SIM Account

Muuaji wa watu 8 na kujeruhi mjini New York afunguliwa mashtaka

Kijana aliyekuwa akiendesha gari lililosababisha ajali kwa kugonga watu Jumanne hii mjini New York na kuuwa watu nane na kujeruhi wengine zaidi ya 12 amefunguliwa mashtaka mahakamani.


Dereva wa gari lililosababisha ajali akiwa ameshika bastola mbili

Dereva huyo aliyefahamika kwa jina la Sayfullo Saipov ambaye ana umri wa miaka 29 na ni raia wa nchini Uzbekstan, anadaiwa kuwa ni miongoni mwa washirika wa kikundi cha kigaidi cha Islamic State.


Picha ya baadhi ya polisi na waokoaji wakikagua maiti za watu waliokufa katika ajali hiyo

Kwa mujibu wa waendesha mashtaka wa New York wamesema, Sayfullo amefunguliwa mashtaka makubwa mawili ambapo la kwanza likiwa ni kutoa msaada kwa kundi la IS na lapili ni kusababisha uharibifu wa magari ambayo yalisabisha vifo na majeruhi.

Wakati huo huo Rais wa Marekani Donald Trump ametaka adhabu kali kutolewa kwa watu wanaobainika kujihusisha na vitendo vya kigaidi ikiwemo hilo lililotokea mjini New York.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW