Burudani

Muziki bado naudai hela nyingi – Z Anto

Msanii wa zamani ‘Z Anto’ aliyewahi kufanya vizuri na wimbo ‘Binti Kiziwi’ amefunguka kwa kudai anarudi kwenye muziki ili kuchukua hela ambayo aliiacha kipindi cha nyuma wakati ambao amedai muziki ulikuwa haulipi vizuri.

Muimbaji huyo ambaye anajipanga kuachia wimbo mpya hivi karibuni, ameiambia Bongo5 kuwa wakati wa nyuma muziki haukuwa unalipa kama wakati huu.

“Kusema kweli wakati ule muziki ulikuwa haulipi kama sasa hivi, sasa hivi muziki unalipa sana, ukiangalia wimbo kama Binti Kiziwi au Mpenzi Jini ni nyimbo ambazo zilitakiwa bado niendelee kula hela yake. Kwahiyo naweza kusema muziki bado haujanilipa hela ambayo nastahili kuipata ndio maana nimeamua kurudi upya ili kuitafuta,” Z aliambia Bongo5.

Aliongeza, “Kwa sasa hivi mimi naona pesa ipo sana ndio maana nimeamua kurudi upya na nguvu mpya kwenye muziki kwaajili ya kupata kile ambacho nilistahili kupata,”

Muimbaji huyo amedai atakuja na kampuni yake mpya ambayo ataipatia jukumu la kisimamia muziki wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents