Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Muziki umekuwa mgumu kuliko zamani – Jay Moe

Msanii mkongwe wa hip hop Bongo, Jay Moe amedai kuwa muziki kwa sasa umekuwa mgumu zaidi ukilinganisha na zamani.

Rapper huyo amesema muziki wa sasa umekuwa na mambo mengi ambayo pia yamechangia kuwaondoa baadhi ya wasanii ambao wana uwezo mkubwa.

“Muziki umekuwa mgumu kuliko zamani, ugumu wake ni kwamba zamani ulikuwa hauhitaji kufanya photo shoot, hauhiaji kuji-brand kwenye mitandao ya kijamii kudeal na video ukitoa tu ngoma kama Jua au Mvua, sijui Kama Unataka Demu tuliprint CD tukasambaza kwenye redio tofauti na tukahit na tukaweza kuisha,” ameiambia XXL ya Clouds Fm na kuongeza.

“Lakini ukizunguzia muziki wa sasa hivi unaona wasanii wakali lakini wanashindwa kuingia ndani yake sababu ya mazingira ya game ilivyo sasa hivi. Game inahitaji vitu vingi, hiyo game huwezi kuifanya mpaka uwe na pesa, mpaka kuwa sign na label kubwa ambayo inaweza kukugharamia,” amesisitiza Jay Moe.

By Peter Akaro

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW