Burudani

Muziki unaendelea na uongozi unaendelea – Jaguar

Msanii kutoka nchini Kenya, Charles Njagua a.k. Jaguar mara baada ya kushinda kiti cha ubunge katika jimbo la Starehe Nairobi, amesema kwake muziki bado unaendelea kwa sababu ndio umefanya watu kumjua.

Jaguar ameeleza licha kufanya hivyo bado atatekeleza majukumu yake kama mbunge kwa kuhakikisha vijana na wasanii wanainuka.

“Nishaingia studio na sasa hivi nilikuwa naongea na prodyuza wangu tutaonana jioni, hivyo ninasema muziki unaendaelea na uongozi unaendelea, sitaacha kutunga nyimbo kwa sababu ndio imefanya watu kuweza kunijua na niendeleze vile vitu nimekuwa nikifanyia kwenye jamii,” ameiambia Mambo Mseto ya Radio Citizen na kuongeza.

“Kwanza kuna wasanii wengi wao walinisapoti na zile shida ambazo tumekuwa tukizipitia nitaenda kuzizungumza bungeni, kwa hiyo nitashirikiana na vijana wenzangu kuhakikisha wasanii na vijana wote mambo yao yanakuwa katika mpangilio,” amesema.

Alipoulizwa kama umaarufu wanaopata wasanii ndio unapelekea wengi wao kushinda pindi wanapogombea nyadhifa za uongozi, Jaguar alisema hilo halina ukweli bali ni namna msanii anavyokuwa karibu na jamii.

“Ni wasanii wengi wamegombea na wakashindwa, usanii pekee hauwezi kukusaidia kwa sababu hauendi bungeni kukatika useme Jaguar amechanguliwa akaimbe huko bungeni, naweza kusema ni vile unakuwa karibu na watu kwa sababu kuna wasanii wanakuwa wakubwa hawaonani na watu lakini kuna yule msanii anajulikana, anabarikiwa na Mungu lakini anarudi kukaa na watu,” amesema.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents