Burudani

Muziki wa Barakah umeshuka – Bright

Msanii wa Bongo Flava, Bright amefunguka juu ya msanii mwenzake Barakah The Prince ambaye alisIkika katika ngoma yake ‘Nitunzie’ kabla ya kuhama ‘lebo’ waliyokuwa wakifanya kazi pamoja.

Akiongea na Bongo5 mapema wiki hii Bright ameeleza kuwa Barakah amekuwa ni msanii wa kuhama menejiment kila mara kitu kinachopelekea muziki wake kuzidi kushuka.

“Mimi nafikiri Barakah ni mwehu kwanza ndio maana anahama hama, haiwezekani mtu upo kwenye menejimenti ukatae kuongozwa lazima kuwe na uongozi ambao lazima uhuheshimu na lazima ukubali kuongozwa, kama unahitaji mahitaji yako na unatimiziwa sasa kwa nini uhame, sijui alikuwa anahitaji nini ila kwa kawaidia Barakah ni mwehu,” amesema Bright.

Pia mkali huyo wa ngoma ya ‘Wasikudanganye’ ameongeza kuwa “Barakah hawezi kuishi na watu,tuseme sijui hajakua, sijui ulimbukeni, sijui anakuaje mimi sielewi ndio maana unakuta graph yake ya muziki inakuwa mbaya, anarudia nyimbo anarudia maneno, anarudia melody, anarudia beat, nafikiri labda muziki umemshinda, kwa hiyo tumuache na kuhama hama kwake kama nahisi kutampa faida au kutampa hasara maana anajua nini anataka.”

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents