Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Muziki wa dansi umekosa tungo wamebaki watumbwizaji – Suzi Batazary (Video)

Mtangazaji wa muziki wa Dansi nchini, Suzi Batazary amesema kuwa mziki huo umepoteza watunzi wa mashairi na sasa wengi waliokuwepo ni watumbwizaji.

“Kwenye upande wa mziki wa dansi tungo zimepungua watu wanaburuza tu. Tungo hakuna kabisa watunzi hawapo katika muda mfupi  wengi wameshaondoka katika hii dunia tumebakiwa  na wakina  Cristian Bela , Nyoshi  waliobaki wengi wanatumbwiza nyimbo kama za kina Tx Moshi William hazipo tena” amesema Suzi Batarazary ambaye ni mtangazaji wa muziki wa dansi.

Batazary ameongeza kuwa “Ukiwa kiongozi katika bendi sio heshima kutembea na watumbwizaji wako ila sio sababu ya msanii kushuka katika mziki, nidhamu yakazi kwa wasanii wa hapa nyumbani imeshuka inapelekea wadau kukimbia na mziki kukosa mashabiki”.

By Hamza Fumo

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW