Burudani

Muziki wangu umekosa mshindani, sina msanii wa kushindana naye – H.Baba

Msanii wa muziki, H.Baba amesema ukimya wake kwenye muziki umesababishwa na kukosa mshindani kwenye aina ya muziki ambao anaufanya.

Muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo kama ‘Mpenzi Bubu’ na nyingine nyingi, amesema ameona akae pembeni kwa muda kuwa muziki wa BongoFleva unaenda kupotea kabisa kwenye ramani nchini Tanzania.

“Mimi binafsi naona muziki unaelekea ukingoni, wasanii wameacha kufanya muziki wanafanya kiki kila kukicha,” alisema H.Baba. “Sisi tulipendwa kutokana na muziki wetu na sio makiki yasio na mpango ndio maana baada ya kuona sina mshindani tena nikaamua nikae pembeni siku akitokea mshindani wangu mtaona fujo zangu,”

Aliongeza,”Wasanii wanaishi maisha ya uongo, anapost picha ana pesa kumbe ameomba kwa jirani akige nazo picha tu lakini ukija kuangalia maisha yake unakuta maisha yake ni magumu sana,”

H.Baba amedai kwa sasa nashindwa kuweka wazi ni lini ataachia wimbo wake mpya kwa madai anaogopa kulogwa kwani wasanii wa siku hizi wanatumia ndumba kuwashusha kimuziki wasanii wenzao.

Kwa sasa unaweza kupata habari zetu zote sehemu moja kwa kupitia App yetu ya Bongo5. Pakua sasa kupitia Play Store kwa kubonyeza link hii – https://bit.ly/2J2Argw

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents