Burudani

Muziki ya Darassa ilivyogeuka wimbo wa taifa ndani ya wiki moja

Hii hutokea kwa nadra sana na tena kwa wasanii wachache tu wenye ngekewa zao. Kama ni soka, basi Darassa amepiga hat-trick. Kama Utanipenda, Too Much na Muziki ni nyimbo zilizobadilisha upepo katika maisha ya muziki ya Darassa.

15101783_554164378116470_9052220755500072960_n

Kama Utanipenda na Too Much zilikuwa ni kama mvua za rasha rasha zilizoashiria kuwa kuna mvua kubwa inataka kunyesha. Bila promo kubwa, Novemba 23, Darassa aliachia wimbo wake Muziki ambao ungekuja kuwa gia ya mwisho wa kuashiria kuwa gari limeondoka rasmi.

Muziki, wimbo ambao amemshirikisha Ben Pol huku kwa mbali ukikopa kionjo cha wimbo wa Saida Karoli, Chambua Kama Karanga na kupewa midundo inayokaribiana na dancehall, umegeuka kuwa wimbo wa taifa ndani ya muda mfupi. Wimbo huu umeyagusa masikio ya watu wa kila rika na wote wanaongea ujumbe mmoja – Darassa ametisha.

Muziki ni club banger usiyoweza kuikwepa kila uendako – mtaani, baa, kwenye bajaj, daladala na kila upigwapo kwenye hadhara si rahisi kujizuia kuusakata kwenye dancing flow. Wimbo huu una rotation kubwa redioni na kwenye TV. Mastaa wenzake pia wanazungumza lugha moja kuwa mwaka huu Darassa amelamba dume.

Akiucheza wimbo huo, mrembo Jokate Mwegelo, alipost video kwenye Instagram na kuandika: Happy Swahili Fashion Week Lovers ????????. Bonge la ngoma wacha nikubali tu mambo ni ????????????????????.”

Naye mrembo mwingine, Elizabeth ‘Lulu’ Michael amepost video akifurahia wimbo huo na kuandika: Mama Micah on the One n Two…Shikamoo @laviemakeup Sio Simba,Sio Chui,Sio Mamba….Kazi Yangu Tu inatosha kujigamba ????Nasikia huu ni Wimbo wa Taifa????.”

“Mimi Wakazi nasema hivi, Ndio Kwa sasa DARASSA is one of the hottest rap artist in the country, period. (Nilikuwa Dodoma na Wimbo wake mpya unafanya vizuri kuliko hata wa Wasafi mpya,” aliandika Wakazi.

Naye producer Jors Bless ameandika: Jamaa ameula bana……. I’m happy he found a style na sound ya kumtambulisha, you listen to nyimbo za Darassa from ile alofanya na Blue I think Heya haye or whatever it’s like from there aliamza kutembea na template ya muziki wake, he found himself….. That’s what wasanii wengi wanafeli, hawajijui wanafit wapi, at the end of the day they want to do everything hence a confusion because there is no identity, darassa found his.”

Ndani ya wiki na nusu, video ya wimbo huu imeshavutia views zaidi ya 788,000 – kitu ambacho ni nadra kwa msanii anayefanya Rap. Umma umeukubali wimbo huu na ni kweli kuwa kile alichokisema katika miongoni mwa nyimbo zake za mwanzo kabisa, ‘Sikati Tamaa’ kimemsaidia kufika hapo alipo leo.

Naamini kuwa Darassa anaelekea kuanza kuifaidi fedha ya muziki ambayo ni wasanii wachache wapo kwenye nafasi hiyo. Kwakuwa kama alivyosema Jors Bless kuwa ametambua sound yake, rapper huyu ataendelea kukwea ngazi na kama ataendelea kutengeneza hits zaidi, Tanzania inaenda kupata msanii mwingine wa rap mwenye ushawishi mkubwa siku za usoni.

Nauona muziki ukitumika kwenye kampeni na matangazo ya biashara ya matangazo makubwa. Kwa jinsi wimbo wake unavyofanya vizuri, rapper huyu hakwepeki kwenye kila tamasha kubwa. Shabiki mmoja anadai kuwa muitikio wa kushangaza wa wimbo wake, unadhihirisha kuwa woga uliopo kuwa timu zinadidimiza muziki wa Tanzania hauna maana. Anaamini kuwa kila msanii atakayeweza kufanya muziki mzuri ana nafasi ya kumega mkate wa tasnia hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents