Burudani

Muziki ya Darassa ilivyoteka ufalme wa Bongo Flava ndani ya mwaka mmoja

Novemba 23 ya mwaka 2016 ilikuwa ni siku ambayo Darassa aliweza kupata tobo kupitia ngoma yake ya ‘Muziki’.

Hakika wimbo huo uliteka Bongo Flava katika kipindi kifupi na kuanza kugeuka kuwa kama wimbo wa taifa.

Hii hutokea kwa nadra sana na tena kwa wasanii wachache tu wenye ngekewa zao. Hali hii ilimfanya msanii huyo kama ni soka, basi alikuwa amepiga hat-trick na kuanza kubadili maisha yake kiulaini kwa kupata show lukuki kila kukicha.

Bila promo kubwa kufanywa wimbo huo uliweza kutoboa na kupenya kwenye masikio ya watu wa rika zote. Lakini kubwa zaidi wimbo huu mpaka sasa umetimiza mwaka mmoja na umefanikiwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 10 katika mtandao wa Youtube.

Huu umekuwa wimbo wa kwanza wa msanii wa Hip Hop hapa Bongo kutazamwa mara nyingi zaidi lakini pia umeweza kutikisa mpaka video nyingi za wasanii wa kuimba ambazo nyingi bado hazijafikia level za ‘Muziki’.

Huwezi kuamini video hii imezizidi mpaka ngoma nyingine zikiwemo za wasanii wa WCB ambao ndio wanaonekana kutazamwa zaidi kutokana na kuwa na wingi wa mashabiki wanaowapa support. Kutoka WCB ni video kadhaa za Diamond na ngoma ya ‘Bado’ ya Harmonize ndio zimefanikiwa kutazamwa mara nyingi zaidi ya wimbo huo wa Darassa.

Lakini kwa upande wa Alikiba ni ngoma yake ya ‘Mwana’ pekee ambayo ilitoka takribani miaka miwili iliyopita na kutazamwa mara milioni 17 ndio imefanikiwa kuizidi ‘Muziki’ ya Darassa.

Nadhani utakuwa unakumbuka Ambwene Yessaya maarufu kama AY aliteka vichwa vya habari baada ya kuachia ngoma yake ya Zigo Remix ambayo alimshirikisha Diamond. Lakini ngoma hiyo bado haijafikia kiwango cha Muziki kutokana na mpaka sasa imeweza kutazamwa zaidi ya mara milioni 9.2 tu.

Hakika huu ndio wimbo ambao Darassa atakuwa anaukumbuka katika maisha yake yote ya muziki kwa kuwa ni nadra sana kwa msanii kutoa hit na kukubalika mpaka nje ya mipaka ya nchi yake hasa kwa msanii kama yeye ambaye amesota kwa muda mrefu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents