Aisee DSTV!

Mvua kubwa yapiga Marekani na kusababisha mafuriko katika jiji la kibiashara Washington DC, magari yakwama

Mvua kubwa imeripotiwa kunyesha hapo jana siku ya Jumatatu, katika jiji la Washington DC nchini Marekani na kusababisha mafuriko na kupelekea hadha kubwa kwa watumiaji wa vyombo vya moto  na waenda kwa muguu kwenye maeneo kadhaa ya barabara.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vimeripoti kuwa maji yameonekana kujaa kwenye sehemu mbalimbali ya jiji hilo ikiwemo White House jambo ambalo linaelezwa kuwa si lakawaida kutokea.

Baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu ya Marekani (White House) wame ‘tweeted’ picha ambazo zinaonyesha maeneo ambayo maji yameingia.

Mamlaka za hali ya hewa zinatazamia kuwa mafuriko hayo ni ya historia katika jiji la Washington DC.

Mvua hiyo iliyonyesha kwa zaidi ya saa 1, katika jiji hilo la kibiashara inakadiriwa kuwa na ukubwa wa mm 88.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW