Habari

Mvua kubwa yasababisha ufa daraja la Dumila, Mabasi ya mikoa ya kanda ya kati yazuiwa kupita (+video)

Daraja la Dumila mkoani Morogoro maarufu kama daraja la Magufuli kwa sasa halipitiki baada ya kujaa maji na kingo zake kuweka nyufa kutokana na mvua kubwa inayonyesha.

Kujaa huko kwa maji kumesababishwa na mvua kali iliyonyesha usiku katika wilaya za Kilosa, Mvomero na mikoa ya jirani ya Tanga na Manyara.

Tayari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa ameyataka magari yote yanayotumia barabara hiyo kutumia njia mbadala ya Mkata mpaka hapo utaratibu mwingine utakapofanyika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents