Habari

Mvulana wa miaka 15 asafiri kwa kujificha kwenye matairi ya ndege kutoka Benin hadi Lagos Nigeria!

Tumezoea kusikia matukio ya watoto wanaodandia mabasi na kujificha sehemu ya mizigo yatokayo mikoani kuja Dar es salaam, lakini huko Nigeria mvulana wa miaka 15 aliwashangaza watu wengi baada ya kukamatwa kwa kudandia ndege na kusafiri akiwa amejificha kwenye matairi ya ndege ya Arik Air kutoka mji wa Benin hadi Lagos.

Arik

Kwa mujibu wa Taarifa ya Reuters, msemaji wa kampuni ya Arik Air, Ola Adebanji jana Jumapili alisema kuwa mvulana huyo aitwaye Daniel Ihekina alipenya na kuingia katika uwanja wa ndege wa Benin Nigeria na kufanikiwa kuwakwepa walinzi kisha kwenda sehemu ya matairi ya ndege hiyo na kufanikiwa kudandia ndege hiyo kabla haijaanza kuruka Jumamosi iliyopita (August 24).

Airk-stowed4

Msemaji huyo amesema kuwa Daniel anabahati kwa kufanikiwa kufika salama kwa sababu ndege hiyo iliruka umbali wa ‘21,000 feet’ kutokana na safari hiyo kuwa fupi ya muda wa nusu saa kutokea mji wa Benin hadi Lagos Nigeria.

Mtandao mwingine wa vanguardngr umesema rubani wa ndege hiyo alidai kumuona mvulana akitokea kichaka cha pembeni mwa uwanja huo na kutoa taarifa kwa ‘Control Tower’ wa uwanja huo wa Benin, ambao walimwabia wanatuma maafisa wa usalama na hivyo kumruhusu kuondoka.

Mmoja wa abiria alisema kuwa wakati ndege inakaribia kuondoka Benin walisikia sauti za kelele kama tairi limemkanyaga mtu na wote wakaanza kupiga kelele za ‘yesu yesu’. “We had the sign in Benin-City when the plane was about leaving. As it was moving slowly, we heard a loud noise as if the tyre crushed somebody on the ground and we all started shouting ‘Jesus, Jesus’. It means the boy was already inside that tyre compartment before we left”.

Baada ya ndege hiyo kutua ndipo mvulana huyo aliruka kutoka kwenye tairi la ndege na kila mtu akaanza kupiga kelele kabla ya maafisa wa usalama kumwona na kumkamata.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents