Burudani ya Michezo Live

Mwakilishi wa La Liga azungumzia usajili wa Eden Hazard, amtaja nyota wa Tanzania Farid Mussa (+Video)

Mwakilishi wa shirikisho la soka nchini Hispania La Liga Santander, Mr. Alvaro Paya hii leo siku ya Jumanne amezungumzia msimu mpya wa 2019/2020 ikiwemo kupanda kwa timu tatu ambazo ni, CA Osasuna, Granada CF pamoja na RCD Mallorca. Usajili wa wachezaji wapya akiwemo Eden Hazard, De Jong na mambo mbalimbali yakiwemo viwanja na VAR.

Mbali na yote, Alvaro Paya amezungumzia kukosekana kwa wachezaji kutoka Afrika Mashariki katika ligi hiyo huku akimgusia mchezaji wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya CD Tenerife B, Farid Mussa.

Kwa upande wa kampuni ya kubashiri matokeo ya michezo SportPesa, Sabrina Msuya ambaye ni Afisa Habari na Mahusiano ameishukuru La Liga kwa ushirikiano wao na kuwataka wachezaji wao kucheza hata kupitia website ya www.sportpesa.co.tz.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW