Burudani ya Michezo Live

Mwakinyo azidi Kilo kabla ya Pambano, mwenyewe adai ni Matunda ”Nilikula Fruti kama glasi sita” (+Video)

Bondia wa Tanzania, Hassan Mwakinyo hii leo siku ya Alhamisi, amepima uzito yeye na mpinzani wake Mfilipino, Arnel Tinampay kuelekea kwenye pambano lao la hapokesho siku ya Ijumaa Novemba 29 mwaka 2019.

Katika zoezi hilo, Mwakinyo ameonekana kuzidi kilo huku mwenyewe akidai ni kutokana na kula glasi sita za ‘Fruti’ kabla ya kufanya vipimo hivyo.

Wakati mpinzani wake, Tinampay akijaribu kupima mara mbili badala ya mara moja kama ilivyozoelekea, huku lengo lake likiwa ni kujiridhisha.

Kuelekea pambano hilo litakalo fanyika uwanja wa Uhuru, hakutakuwa na kiingilio chochote bali kila mtu atakayehudhuria atalazimika kuwa na tiketi ambayo ataipata pale pale wakati mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW