Soka saa 24!

Mwakyembe: Marufuku kuchimba dawa njiani!


Kama una mpango wa kusafiri kuelekea mikoani siku za hivi karibuni, jipange kupanda basi ukiwa umerekebisha haja ndogo mapema kabisaaa, kwakuwa utajuta mbeleni, hakuna kuchimba dawa tena, habari ndio hiyo!
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amepiga marufuku kuanzia sasa kwa mabasi ya abiria yaendayo mikoani kusimama eneo lolote njiani kwa madhumuni ya abiria kujisaidia haja ndogo maarufu sana kama ‘kuchimba dawa’.
Akizungumza wakati wa kutoa pendekezo la kuungwa mkono na wabunge kwa bajeti ya wizara yake, Mwakyembe alisema endapo basi litaonekana barabarani limepaki kwa ajili ya kuchimba dawa litafungiwa leseni.
Amesema jambo hilo humdhalilisha mwanamke ambaye amezaliwa na umbile la kujisitiri na pia hushusha heshima kwa wazazi.
Waziri huyo alisema abiria wote wanatakiwa kutumia nafasi hiyo kwenye vituo vikubwa wanavyosimama.
“Tutatoa onyo kwa mara ya kwanza,ya pili kama hatutajirekebisha basi tunachukua maamuzi[uamuzi] wa kumfungia leseni,kumuona mama yako anajisaidia ni sehemu ya kujilaani,hatuwezi kudhalilisha hivyo mama zetu,huo si utamaduni wetu” alisema Mwakyembe (Mwananchi).
Biashara ya juice njiani sasa imepata pigo!!!!

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW