Aisee DSTV!

Mwalimu ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kulawiti, Mahakama yaamuru apigwe kwanza viboko kabla ya kutupwa jela

Kijana Charles Msele (32) ambaye pia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya Rift valley English Medium and Primary School iliyopo Babati mjini mkoani Manyara, Amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kulawiti.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Manyara, Simon Kobero, amesema adhabu hiyo imetolewa baada ya mtuhumiwa kutiwa hatiani.

“Mtuhumiwa alimlawiti mtoto wa kiume wa miaka 11 mwanafunzi wa darasa la tano wa shule hiyo ambapo tukio hilo lilitokea shuleni hapo kwenye bweni la watoto wa kiume,”

Imeelezwa kuwa mtuhumiwa alimuita  mtoto huyo bwenini na baada ya  hapo na yeye alienda akiwa na vilainishi aina ya femo pamoja na mafuta ya mgando aina ya Baby soft, ambapo baada ya kufika bwenini mtuhumiwa alimpaka mafuta hayo kwenye  sehemu za haja kubwa kisha yeye kujipaka sehemu zake za siri na kumlawiti.

Mtuhumiwa alifikishwa mahakamani Oktoba 8, 2019 kwa mara ya kwanza ambapo alisomewa shtaka lake na kukana,  baada ya kukana kosa hilo shauri liliendelea kwa hatua ya usikilizwaji.

Upande wa mashtaka ulisema kuwa mshtakiwa ametiwa hatiani, Ambapo mwendesha mashtaka Wakili wa serikali Petro Ngassa, aliomba mtuhumiwa apewe adhabu kali pamoja na kutoa fidia kwa muhanga kutokana na kitendo alichokifanya.

Mtuhumiwa aliomba apunguziwe adhabu hiyo bila kutoa sababu yoyote na ndipo mahakama ilipomuhukumu kifungo cha maisha jela lakini pia kuchapwa viboko vinne kwenye makalio na kulipa fidia kwa mhanga kiasi cha Tsh. milioni 3.

Chanzo: Gazeti la Mtanzania

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW